Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waasi Ethiopia waunda muungano dhidi ya serikali ya Abiy

WAASI.png Waasi Ethiopia waunda muungano dhidi ya serikali ya Abiy

Sat, 6 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makundi tisa yanayoipinga serikali ya Ethiopia kikiwemo chama cha Tigray People’s Liberation Front yamekubali kuunda muungano dhidi ya utawala wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed. Inakuja huku shinikizo zikiongezeka kwa Bw Abiy, huku vikosi vya waasi vikipiga hatua kuelekea mji mkuu. Lakini serikali ya Addis Ababa imesema inakaribia kupata ushindi na itaendelea kupigana kile inachokiita kuwa ni vita vilivyopo.

Washirika wa kimataifa wa Ethiopia wametoa wito wa kukomesha uhasama huo. Mjumbe Maalum wa Marekani katika Upembe wa Afrika yuko Addis Ababa na amefanya mikutano na mawaziri wa serikali.

Msemaji wa Jeshi la Ukombozi la Oromo ambalo ni sehemu ya muungano mpya wa kijeshi na kisiasa aliiambia BBC kuwa lengo lao ni kuondoa serikali ya sasa ya Ethiopia, kuanzisha utawala wa mpito na baadaye kufanya mazungumzo kuainisha mustakabali wa Ethiopia.

Makundi mawili ya waasi wa Oromo na Tigray People’s Liberation Front tayari yameanza kupigana pamoja na wiki hii yalidai kuuteka mji wa Kemise kilomita 325 kaskazini mwa Addis Ababa.

Tangazo rasmi litatolewa Ijumaa asubuhi huko Washington DC. Lakini hatua hii inaweza kudhoofisha juhudi za Mjumbe Maalum wa Marekani katika Upembe wa Afrika Jeffrey Feltman ambaye ameanza kukutana na mawaziri wa serikali ya Ethiopia kushinikiza mazungumzo. Pande zote mbili katika mzozo huu zinaendelea kukataa wito wa kusitisha operesheni zao za kijeshi.

"Lengo ni kuondoa udikteta wa Abiy ambapo baada ya hapo serikali ya mpito itaanzishwa na mazungumzo yatafanyika na washikadau wote ili kuweka ramani ya mustakabali unaokubalika kwa wote." - Odaa Tarbii, Msemaji wa OLA

Vikundi vinavyotarajiwa kujiunga na Muungano huo wa

United Front of Ethiopian Federalist and Confederalist Forces alliance ni:

Oromo Liberation Army, Tigray People’s Liberation Front, Sidama National Liberation Front, Somali State Resistance, Afar Revolutionary Democratic Unity Front, Agaw Democratic Movement, Benishangul People's Liberation Movement, Gambella Peoples Liberation Army, Global Kimnt People Right na Justice Movement/ Kimant Democratic Party.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live