Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waasi ADF waihama ngome yao kufuatia mashambulizi ya kijeshi ya Uganda na DRC

Waasi ADF Waasi wa ADF

Fri, 18 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waasi wa ADF ambao wameshtumiwa kuendeleza maafa ya maelfu ya raia Mashariki mwa DRC kwa sasa wanahamia maeneo ya Magharibi kutoka kwenye ngome yao, karibu na mpaka wa Uganda.

Hatua hii inaelezwa na wachambuzi wa masuala ya vita, kufuatia operesheni za kijeshi zinazoongozwa na Uganda tangu mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2021.

Kwa kipindi cha wiki moja pekee, katika Wilaya ya Beni huko Kivu Kaskazini na Irumu, mkoani Ituri, raia 79 wameuawa baada ya waasi hao kuvamia vijiji sita.

Tangu mwaka 2019, Wilaya ya Irumu ndio iliyoathiriwa zaidi, tangu kundi hilo lianze mashambulizi dhidi ya raia, lakini Beni pia imekuwa ikishambuliwa tangu mwaka 2014.

Mbunge kutoka Goma Jean-Baptiste Muhindo Kasekwa, anasema kati ya Machi 9 mpaka 14, watu 96 wameuawa Wilayani Beni na Irumu, wengine 383 tangu operesheni za jeshi la Uganda na zaidi ya Elfu mbili tangu kuanza kutekelezwa kwa hali ya dharura katika maeneo hayo mwezi Mei mwaka uliopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live