Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waangalizi wa Umoja wa Ulaya wakosoa uchaguzi wa Nigeria

Waangalizi Wa Umoja Wa Ulaya Wakosoa Uchaguzi Wa Nigeria Waangalizi wa Umoja wa Ulaya wakosoa uchaguzi wa Nigeria

Tue, 28 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya umekosoa ukosefu wa uwazi na kushindwa kwa utendaji katika uchaguzi wa Nigeria, kulingana na matokeo yake ya awali.

Ilisema kuna imani katika uhuru na weledi wa chombo cha uchaguzi wakati wa maandalizi ya uchaguzi huo. Lakini imani ya umma ilipungua kutokana na kukosekana kwa mipango madhubuti na mawasiliano madhubuti katika mchakato huo - ikiwa ni pamoja na siku ya uchaguzi, waangalizi walisema.

Raia wa Nigeria walipiga kura zao katika uchaguzi mkuu wa rais na wabunge siku ya Jumamosi.

Waangalizi hao walibaini kuwa baadhi ya vituo vya kupigia kura vilichelewa kufunguliwa na taratibu za upigaji kura hazikufuatwa kama ilivyotakiwa.

Walisema upakiaji wa matokeo kwa kutumia mfumo wa kielektroniki haukufaulu, hivyo kuzua wasiwasi kwani uwasilishaji wa fomu za matokeo ya uchaguzi wa urais ulicheleweshwa.

Timu ya waangalizi hao imewataka wadau katika uchaguzi huo kuzingatia amani hadi mchakato huo utakapokamilika na kutaka migogoro itakayojitokeza ishughulikiwe kwa njia za kisheria.

Chanzo: Bbc