Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waangalizi Kimataifa wakoshwa uchaguzi Liberia

Liberia Msl Waangalizi Kimataifa wakoshwa uchaguzi Liberia

Sat, 18 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa nchini Liberia, wameipongeza nchi hiyo kwa kufanya uchaguzi wa amani wa duru ya pili, wakati huu wagombea wawili rais George Weah na mpinzani wake Joseph Boakai, wakikaribiana kwa kura.

Matokeo ya awali yanaonesha kiongozi wa upinzani Joseph Boakai anaongoza kwa asilimia 50.58 dhidi ya Rais George Weah ambaye ana asilimia 49.42.

Katika duru ya kwanza, wagombea hao walishindwa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zote, hii ikiwa ni kama marudio ya uchaguzi wa mwaka 2017 ambapo baada ya duru ya pili, Weah aliibuka mshindi kwa zaidi ya asilimia 61 ya kura.

Uchaguzi wa mwaka huu ni wa kwanza tangu Umoja wa Mataifa ulipohitimisha ujumbe wa kulinda amani nchini Liberia.

Ujumbe huo uliundwa baada ya zaidi ya watu 250,000 kufariki katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1989 na 2003.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live