Alhamisi wakati wa maandamano ya kitaifa yaliyoitishwa na mrengo wa pinzani, Azimio, matukio mbalimbli yasiyorufahisha yaliripotiwa katika sehemu mbalimbali za nchi.
Katika kaunti ya Kisumu, tukio la ajabu ambalo limezidi kuteka vichwa vya habari ni lile baada ya waandamanaji kuvamia chumba cha kuhifashi maiti.
Waandamanaji wa Azimio walifanya maandamano siku ya Alhamisi na kuvamia chumba kipya cha kuhifadhia maiti kilichofunguliwa katika Hospitali ya Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga (JOOTRH), kuiharibu na kuiba vitu vya thamani ya mamilioni ya pesa.
Wakazi wa Kisumu hawakuwaacha hata wafu ambao wamekuwa wakilala kimya na kuganda ndani ya chumba cha maiti.
Waasi hao waliharibu gari la kubebea maiti na kusafirisha vifaa vikiwemo toroli na kompyuta.
Wengine walibeba fanicha zilizokuwa zimewekwa kwenye chumba cha mapumziko cha jumba la wafu la Shilingi milioni 37 ambalo lilifunguliwa rasmi siku mbili zilizopita.
Wasumbufu hao walidai kuwa mwanafunzi wa shule ya upili aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi na mwili wake kuhamishwa na polisi hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha JOOTRH.
Walakini, hadi wakati wa mkutano na waandishi wa habari, mwanafunzi aliyepigwa risasi alikuwa bado hospitalini.
Wafanya ghasia hao walipovamia kituo hicho, walinyimwa fursa ya kuutazama mwili huo unaodaiwa kuwa jambo lililowakasirisha.
Kufikia saa majira ya jioni, waandamanaji walikuwa bado wanazunguka kituo hicho wakitarajia kupora vitu zaidi kutoka kwa kituo hicho, walioshuhudia walisema.
Gavana wa Kisumu, Prof Anyang' Nyong'o alikashifu kuharibiwa kwa jumba la maiti akidai mafisadi waliojifanya kama waandamanaji ndio waliovunja lango lililoharibiwa na kupora vifaa vya bei ghali vya chumba cha kuhifadhia maiti alichozindua wiki jana.
Alielezea shambulio hilo katika nyumba mpya ya mazishi, ya kwanza ya aina yake huko Nyanza, kuwa la kikatili na kihuni.