Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waandamanaji wasambaza majeneza Nairobi

Majeneza Ms(1).png Waandamanaji wasambaza majeneza Nairobi

Thu, 4 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati vijana wa Kenya wakitekeleza kile walichomuahidi Rais wa taifa hilo, Wiliam Ruto kwamba wanarejea kwenye maandamano kuanzia leo Jumanne, awamu hii wamekuja kwa namna tofauti baada ya kushuhudiwa wakisambaza majeneza katika moja ya barabara maarufu jiji la Nairobi. 

Licha ya kwamba majeneza hayo zaidi ya 10 hayajatambulika kama ndani yake yana miili au lah, tukio hilo limetajwa kuwaacha wakenya wengi na mshangao.

Maandamano hayo ambayo yanaelekezwa dhidi ya serikali na haswa uongozi wa Rais Ruto, wengine wakishinikiza kung’atuka kwake madarakani kama rais.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo jambao la kushangaza ni kwamba wakati polisi wanahaha juu na chini kuwatuliza waandamanaji kwa kuwasambaratisha kwa kutumia mabomu ya machozi, wengine walitokea kusikojulikana wakiwa wamebeba majeneza na kuyaweka katikati ya barabara.

Tukio hili liliwaacha polisi kwa mshangao wasijue cha kufanya mara moja kabla ya kuanza kuyainua na kuyaweka ndani ya lori moja la rangi nyeupe.

Baadhi ya waandamanaji walionekana wakitokea katika barabara mbalimbali karibu na bustani ya Jevanjee wakiwa na majeneza hayo kabla ya kuyatelekeza katikati mwa barabara ya Moi Avenue.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live