Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waandamanaji wasababisha hasara ya Mil. 700 Kenya

Waandamanaji Wasababisha Hasara Ya Mil. 700 Kenya .png Waandamanaji wasababisha hasara ya Mil. 700 Kenya

Thu, 13 Jul 2023 Chanzo: Radio Jambo

Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen amesema kuwa uharibifu uliofanywa katika Barabara ya Nairobi Expressway unaweza kuwa zaidi ya Sh700 milioni.

Akizungumza siku ya Alhamisi wakati wa ziara ya kutathmini uharibifu uliosababishwa na waandamanaji, Murkomen alisema thamani hiyo ilifikiwa baada ya kupitia yote yaliyoharibiwa.

Waziri huyo alisema wizara yake imesikitishwa na waandalizi wa maandamano hayo wanaodai kupambana na gharama ya juu ya maisha.

"Kutoka kwa Wizara ya Barabara na Uchukuzi, tumesikitishwa na waandaaji wa hafla ya jana kama ilivyotangazwa na tumetathmini uharibifu.

"Watu ambao wamekuwa wakiandaa hafla hii ya halaiki wameliambia taifa kuwa wanafanya hivyo kwa sababu wanataka kupambana na gharama ya maisha lakini uharibifu uliofanywa kwenye Barabara ya Express kwa muda huo mfupi unaweza kuwa dola milioni 5 (Sh706 milioni). ," Murkomen alisema.

Waziri wa Uchukuzi alibaini kuwa ni mlipa ushuru yule yule ambaye Upinzani unadai kupigania kupunguzwa kwa gharama ya maisha ndiye atakayelipa uharibifu huo.

Murkomen aliwahakikishia wawekezaji wa Expressway kwamba wahusika watachukuliwa hatua.

Waandamanaji Jumatano waliondoa kizuizi cha Expressway karibu na Mlolongo.

Walionekana wakivuta kizuizi kwa nguvu ili kukiondoa.

Baadhi yao walipokuwa wakivuta kizuizi, wengine walikuwa wakiruka na kupiga kelele, huku wengine wakiharibu vyombo vya maua vilivyokuwa kwenye kuta za Expressway.

Usafiri pia ulikwama kwa muda katika Barabara Kuu ya Mombasa huku waandamanaji wakifunga barabara.

Maandamano hayo yalikuwa yameitishwa na Azimio la Umoja, kufuatia harama ya juu ya maisha.

Chanzo: Radio Jambo