Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waandamanaji wapora vitu muhimu vya mahakama

POLISI KENYA DG Waandamanaji wapora vitu muhimu vya mahakama

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idara ya mahakama imesitisha kwa muda shughuli za mahakama mjini Eldoret baada ya waandamanaji kuvamia na kuteketeza mali na kumbukumbu zote za mahakama ya kaunti hiyo siku ya Jumanne Juni 25.

Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa katika eneo hilo Cheronoh Maurine Kesse alisema, Mahakama hiyo imepoteza faili zote, kompyuta na hati nyingine muhimu katika majengo yaliyoharibiwa.

Kesse alisema kutokana na hasara hiyo na hali ya usalama kwa baadhi ya watumishi wa mahakama, uamuzi umefikiwa kusimamisha shughuli zote za mahakama.

Alisema walikuwa wakitafakari njia rahisi ya kurejesha huduma hizo haraka iwezekanavyo.

Mahakama Kuu katika mji huo iko karibu na Maktaba ya Kitaifa ambayo iliharibiwa sana na kuporwa na waandamanaji.

Kesse alisema majaji na wafanyakazi wa mahakama walilazimika kuhamishwa kwa kutumia gari la wagonjwa wakati wa maandamano hayo.

Kesse aliwahakikishia wananchi na watumiaji wa mahakama kuwa mahakama itaanza kazi katika eneo hilo haraka iwezekanavyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live