Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waandamanaji wapigwa mabomu ya machozi Sudan

12989 Maandamano+pic Waandamanaji wapigwa mabomu ya machozi Sudan

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vikosi vya usalama nchini Sudan vimerusha vitoa machozi kwa waandamanaji ambao wanapigania demokrasia katika mji mkuu wa Khartoum.

Walimu waliokuwa wakishiriki katika mojawapo ya maandamano hayo walikamatwa na vikosi vya usalama.

Usiku kucha , waandamanaji waliweka vizuizi kwa siku mbili za kwanza za maandamano ili kupinga mapinduzi ya kijeshi ya mwezi uliopita.

Wanataka serikali ya kijeshi kujiuzulu na kuruhusu mabadiliko ya amani.

Maandamano hayo yanafanyika huku wapatanishi wa Muungano wa mataifa ya Kiarabu {Arab League} wakiwasili mjini Khartoum kwa mazungumzo ili kujaribu kusitisha tatizo hilo.

Waziri mkuu Abdalla Hamdok, bado amewekwa katika kifungo cha nyumbani na anakabiliwa na shinikizo kutoka kwa wanajeshi hao kushirikiana nao, mwandishi wa BBC Andrew Herding amesema kutoka mji huo mkuu.

Mwezi uliopita , kiongozi wa mapinduzi hayo Jenerali Abdel Fattah al – Burhan , alifutilia mbali utawala unaoongozwa na raia , kuwakamata viongozi wa kiraia na kutangaza hali hatari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live