Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waandamanaji wanaopinga LGBTQ watoa wito kufutwa kazi kwa majaji wa Kenya

Waandamanaji Wanaopinga LGBTQ Watoa Wito Kufutwa Kazi Kwa Majaji Wa Kenya Waandamanaji wanaopinga LGBTQ watoa wito kufutwa kazi kwa majaji wa Kenya

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Maandamano dhidi ya wapenzi wa jinsia moja yamefanyika nje ya Mahakama ya Juu katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Mashirika kadhaa ya kiraia na makundi ya kidini yanaelezea kukasirishwa na uamuzi wa hivi majuzi ambao unaruhusu mashirika ya LGBTQ kujiandikisha nchini.

Baadhi ya waandamanaji walibeba mabango ya kuwataka majaji wa Mahakama ya Juu kujiuzulu.

Miaka kumi iliyopita shirika lililofadhiliwa na serikali lilikataa kusajili shirika la kutetea haki za LGBTQ likisema kwamba shirika hilo linaendeleza tabia ya watu wa mapenzi ya jinsia moja katika nchi ambayo mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria.

Hata hivyo majaji mwaka huu walibatilisha uamuzi huo.

Rais wa Kenya William Ruto amewataka viongozi wa kidini kuendeleza kile anachotaja kuwa maadili ya kitamaduni.

Chanzo: Bbc