Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waandamanaji wa upinzani wapambana na vikosi vya usalama

Waandamanaji Wa Upinzani Wapambana Na Vikosi Vya Usalama Waandamanaji wa upinzani wapambana na vikosi vya usalama

Tue, 30 May 2023 Chanzo: Voa

Dazeni ya waandamanaji walipambana na vikosi vya usalama katika mji mkuu wa Senegal, Dakar, Jumatatu baada ya wabunge na wafuasi wao kuzuiwa kutembelea nyumba ya kiongozi maarufu wa upinzani ambaye ana mashitaka ya ubakaji na kukashifu.

Polisi walifyatua gesi za kutoa machozi kwa waandamanaji ambao waliweka vizuizi katika moja ya barabara kuu za Dakar, na katika kitongoji kimoja walichoma gari na kuwasha moto kwenye jengo la wizara.

Ni tukio la sasa kabisa katika miezi kadhaa ya kutokuwepo na utulivu kulikosababishwa na rais Mcky Sall kukataa kutogombea muhula wa tatu na uwepo wa kesi mahakamani zinazo muhusu mpinzani wake Ousmane Sonko.

Hata hivyo Sonko, amepinga shutuma zinazo mkabili akisema zinania ya kumuondoa asigombanie urais katika uchaguzi ujao wa mwezi Febuari.

Chanzo: Voa