Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waandamanaji Afrika Kusini Wapora Chanjo za Covid

Afrika Kusini 1?fit=700%2C467&ssl=1 Waandamanaji Afrika Kusini Wapora Chanjo za Covid

Thu, 15 Jul 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Waandamanaji Afrika Kusini Wapora Chanjo za Covid July 15, 2021 by Global Publishers



Mamlaka ya Usimamizi wa Maduka ya Madawa Afrika Kusini (SACP), imeelezwa kusikitishwa kwake na vitendo vya waandamanaji nchini Afrika Kusini, kuvunja maduka ya madawa na kupora chanjo za Corona katika Majimbo ya Gauteng na Kwa Zulu Natal nchini Afrika Kusini.

Kiongozi wa SACP, Vincent Tlala amesema wamesikitishwa na jinsi serikali ilivyoshindwa kutoa ulinzi kwenye maduka hayo ya madawa, hasa katika kipindi hiki ambacho wimbi la tatu la maambukizi ya Corona limeshika kasi nchini humo.

Tlala amesema kwamba ripoti zinaonesha kwamba zaidi ya maduka ya madawa 90 yamevamiwa na kuporwa madawa mbalimbali zikiwemo chanjo za Corona na kuongeza kwamba hali ni mbaya zaidi katika Jimbo la Kwa Zulu Natal.

Ameongeza kwamba jambo baya zaidi ni kwamba chanjo na dawa nyingine za Corona, hazipaswi kutumiwa bila maelekezo na uangalizi wa karibu wa madaktari, hivyo wana wasiwasi kwamba huenda afya za wote watakaotumia chanjo na dawa hizo kienyeji, zikawa hatarini na kuwataka wananchi kutotumia dawa hizo kiholela mitaani.

Wakati huohuo, Taasisi ya Kupambana na Magonjwa ya Kuambukiza nchini Afrika Kusini (NICD), imesema imepokea ripoti mpya inayoonesha kuwepo kwa visa vipya 17,489 vya Corona na kuongezeka kwa vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo hadi kufikia 65,595.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa taasisi hiyo, inaeleza kwamba maandamano yanayoendelea nchini humo, yamesababisha kukwama kwa mpango wa serikali ya nchi hiyo uliokusudia kutoa chanjo kwa wastani wa watu 200,000 katika siku chache zijazo.

Jeshi la polisi nchini Afrika Kusini limesema mpaka Julai 14, 2021 jumla ya watu 72 walikuwa wamepoteza maisha kufuatia maandamano makubwa yanayoendelea nchini humo, ya kushinikiza kuachiwa kwa rais wa zamani wa nchi hiyo, Jacob Zuma anayetumikia kifungo cha miezi 15 jela kwa kudharau mahakama.

Taarifa kutoka jeshi hilo zimeendelea kueleza kwamba hivi sasa maandamano hayo, yamebadilika na kuwa uporaji na uharibifu wa mali, hasa katika majimbo mawili ya Kwa Zulu Natal na Gauteng.

Share this:TweetWhatsApp Related

Chanzo: globalpublishers.co.tz