Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waandamana kupinga makubaliano ya jeshi na makundi ya kisiasa

Sudan Waandamanannaa Waandamana kupinga makubaliano ya jeshi na makundi ya kisiasa

Thu, 9 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maelfu ya watu wameandmana nchini Sudan kupinga makubaliano yaliyofikiwa baina ya jeshi na makundi ya kiraia na kisiasa ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, maelfu ya watu waliandamana jana jioni katika mji wa Omdurman, magharibi mwa Khartoum kupinga makubaliano kati ya jeshi na makundi ya kiraia.

Waandamanaji walijaribu kufika makao makuu ya bunge huko Omdurman, lakini vikosi vya usalama viliwazingira na kuwatawanya kwa kurusha mabomu ya sauti na vitoa machozi.

Waandamanaji hao waliokuwa wamebeba bendera za Sudan, walipiga nara dhidi ya jeshi na muungano wa kisiasa na kiraia wa "Uhuru na Mabadiliko", na kutaka serikali kamili ya kiraia iundwe nchini humo.

Kwa mujibu wa duru za habari, waandamanaji walikuwa na mabango yaliyosomeka, "La, kwa utawala kijeshi," "La kwa mapatano ya kisiasa," "La kwa Mpango wa Makubaliano" na "Ndiyo kwa utawala wa kiraia wa kidemokrasia". Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan

Vyanzo vya habari hapo awali vilitangaza kusainiwa makubaliano kati ya makundi ya kiraia na baraza tawala la kijeshi la Sudan ili kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo.

Shirika rasmi la habari la Sudan lilitangaza kuwa, makubaliano hayo ambayo yamepangwa kuwa msingi wa kutatua mgogoro wa sasa wa kisiasa nchini Sudan yametiwa saini mjini Khartoum mbele ya maafisa wa ndani, kieneo na kimataifa kati ya makundi ya kiraia na Baraza la Uongozi la Mpito la Sudan.

Makundi hayo yameafikiana kuhusu kipindi cha mpito cha miezi 24 ambacho kitaanza wakati waziri mkuu wa mpito atakapochaguliwa. Kulingana na makubaliano hayo, utawala huo wa mpito utakuwa na viongozi watupu wa kiraia na utakuwa wa kidemokrasia bila ushiriki wa jeshi.

Mkutano wa utiaji saini makubaliano hayo ya kisiasa uliofanyika nchini Sudan ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Marekani, Uingereza, Saudi Arabia, Muungano wa Falme za Kiarabu na Umoja wa Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live