Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waamuzi Uganda kuchezesha Afcon

Ee1f71a6af1fe07cfe88bc4536e9ee83 Waamuzi Uganda kuchezesha Afcon

Tue, 3 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAAMUZI wanne wa Uganda wameteuliwa na Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) kuchezesha mchezo namba 104 kati ya wenyeji Lesotho dhidi ya Benin utakaofanyika Novemba 17, imeelezwa.

Mchezo huo wa kufuzu wa Kundi L utafanyika kwenye Uwanja wa Setsoto katika jiji la Maseru, Lesotho katika nchi hiyo iliyopo Kusini mwa Afrika.

Waamuzi hao ni pamoja na Ali Sabila Chelanget (mwamuzi wa kati), Dick Okello (msaidizi wa kwanza), Isa Masembe (msaidizi wa pili) na William Oloya (mwamuzi wa akiba).

Waamuzi hao wanne wamepiga kambi katika Kituo cha Ufundi cha Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa), Njeru ambako wamekuwa wakichezesha mechi za mtoano za ligi ya Uganda tangu Machi 17, 2020.

Gay Mokoena wa Afrika Kusini ndiye atakayekuwa kamisaa wa mchezo huo wakati Mzimbabwe, Felix Onias Tanagwarima ndiye atakayewatathimini waamuzi.

Baada ya mechi mbili, Lesotho iko katika nafasi ya tatu katika msimamo baada ya kuambulia pointi moja, sawa na Sierra Leone inayoshikilia mkia.

Kabla ya Novemba 17, 2020, Lesotho itacheza ugenini dhidi ya Benin katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Stade Charles de Gaulle huko Port Novo Novemba 14, 2020.

Waamuzi wa mchezo huo:

Mwamuzi: Ali Sabila Chelanget (Uganda)

Mwamuzi wa kwanza: Dick Okello (Uganda)

Mwamuzi msaidizi wa pili: Isa Masembe (Uganda)

Mwamuzi wa akiba: William Oloya (Uganda)

Kamisaa: Gay Mokoena (South Africa)

Mtathmini wa waamuzi: Felix Onias Tangawarima (Zimbabwe)

Chanzo: habarileo.co.tz