Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waafrika wote sasa kuingia Rwanda bila visa

Waafrika Wote Sasa Kuingia Rwanda Bila Visa Waafrika wote sasa kuingia Rwanda bila visa

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameanzisha safari zisizohitaji visa kwa Waafrika wote, na kuifanya Rwanda kuwa nchi ya nne barani Afrika kufanya hivyo.

“Pia tumeondoa vizuizi vya visa kwa raia wa kila nchi ya Afrika pamoja na mataifa mengine mengi.Mwafrika yeyote anaweza kupanda ndege hadi Rwanda wakati wowote anaotaka na hatalipa chochote kuingia nchini mwetu” Rais Kagame alisema siku ya Alhamisi.

Aliongeza kuwa hatua hiyo inalenga kufaidisha soko la utalii barani Afrika linalokua, likipigwa jeki na ukuaji wa uchumi wa kati barani humo.

Rwanda imekuwa kwenye kampeni ya kukuza sekta yake ya utalii, ikishirikiana na vilabu vya soka kama Arsenal na Bayern Munich ili kuitangaza nchi hiyo kama kivutio cha watalii.

Rwanda sasa inaungana na Ushelisheli, Gambia na Benin, nchi pekee za Kiafrika zinazotoa visa bila malipo kwa raia wote wa Afrika.

Wiki hii, Rais wa Kenya William Ruto alitangaza kuwa nchi hiyo itamaliza masharti ya visa kwa wageni wote wa Kiafrika ifikapo 2024.

Nchi kadhaa za Afrika pia zimeingia makubaliano baina ya nchi mbili za usafiri wa bila visa, hivi karibuni Ghana na Afrika Kusini, na Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Chanzo: Bbc