Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WHO yatoa muongozi mifumo ya afya Afrika

Upasuajiiii (600 X 398) WHO yatoa muongozi mifumo ya afya Afrika

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa, usambazaji umeme kwa kiwango kikubwa katika vituo vya afya vya vijijini kwenye nchi zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara ni muhimu katika kukuza uwezo wa bara la Afrika wa kukabiliana na miripuko ya magonjwa mbalimbali.

Salvatore Vinci, mshauri wa nishati endelevu wa WHO amesema kuwa, kuwepo umakini na ubora wa huduma za afya kwa watu wote barani Afrika na sehemu kubwa ya Kusini mwa Dunia, kutategemea kuunganishwa vituo vya afya na nishati ya umeme ili kusaidia ufanisi wa kazi zake kama vile maeneo ya kuhifadhia chanjo na kuendesha mashine za kwenye maabara ya kuchukulia vipimo vya magonjwa mbalimbali.

Ametilia mkazo wajibu wa kuwekezwa sana katika upatikanaji wa nishati ya kuaminika na amezitaka serikali za nchi husika pamoja na wafadhili kuziba pengo la kukosekana umeme wa uhakika barani Afrika.

Vinci pia amesema kuwa, asilimia 15 ya vituo vya afya vya nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara bado havina umeme, na jambo hilo linadhoofisha jitihada za kupunguza mzigo wa magonjwa unaochochewa na umaskini, vita na majanga ya hali ya hewa.

Ameongeza kuwa, umeme wa kutumia nishati ya jua kwenye vituo vya afya barani Afrika ni muhimu sana katika kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga kwani umeme utaweza kuboreshwa huduma za uzazi na chanjo.

Vilevile amesema, kwa kutumia vyanzo vya nishati safi ikiwa ni pamoja na jua na upepo, nchi zinazoendelea barani Afrika zitafaidika na mifumo ya afya ya kuweza kukabiliana na majanga mengi yanayohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live