Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WHO yaonya kuongezeka kwa mzozo wa kibinadamu wa Sudan

WHO Yaonya Kuongezeka Kwa Mzozo Wa Kibinadamu Wa Sudan WHO yaonya juu ya kuongezeka kwa mzozo wa kibinadamu wa Sudan

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Shirika la Afya Duniani (WHO) linaonya kuhusu kuongezeka kwa mgogoro wa kibinadamu nchini Sudan ambapo zaidi ya theluthi mbili ya hospitali za nchi hiyo hazina huduma.

Ripoti zinazoongezeka za mashambulizi dhidi ya vituo vya afya na wafanyakazi.

Kulingana na WHO, milipuko ya magonjwa - ikiwa ni pamoja na malaria, surua na dengue - ambayo ilikuwa imedhibitiwa vyema kabla ya mzozo wa sasa, inaongezeka kutokana na kukatizwa kwa huduma za msingi za afya ya umma.

Pia inasema kuna ripoti zinazoongezeka za unyanyasaji wa kingono na kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana.

Juhudi kadhaa za mazungumzo ya amani zimefanywa lakini hazijafanikiwa kusitisha vita.

WHO imetoa wito kwa pande zote zinazopigana kuwalinda raia, watoaji huduma za kibinadamu na vituo vya afya.

Chanzo: Bbc