Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WHO na Sudan Kusini zaimarisha mapambano dhidi ya magonjwa ya kitropiki

Utafiti: Ugunduzi Wa Bahati Utakavyosaidia Kupambana Na Malaria WHO na Sudan Kusini zaimarisha mapambano dhidi ya magonjwa ya kitropiki

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Afya Duniani (WHO) na serikali ya Sudan Kusini zimeungana kuendeleza mapambano dhidi ya magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika ambayo yanatishia sana afya za wananchi wa nchi hiyo.

Katibu Mkuu katika Wizara ya Afya ya Sudan Kusini, Ader Macar Aciek amesema kuwa, nchi yake kwa kusaidiana na shirika la WHO na washirika wengine, imefanya jitihada nyingi kwa miaka kadhaa sasa ili kukabiliana na tishio la magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika kwa kutoa dawa na kuchukua hatua madhubuti za kumaliza magonjwa hayo.

Amesema wanafanya kazi kwa kushirikiana na pande za kigeni ili kuifikia jamii yote nchini humo na kuhakikisha kuwa watu walioko kwenye hatari wanapata matibabu na kinga dhidi ya magonjwa haya.

Kwa mujibu wa WHO, magonjwa 19 kati ya 20 yaliyopuuzwa ya kitropiki nchini Sudan Kusini yameenea sana nchini humo. Zaidi ya watu milioni 12 wako katika hatari ya kuambukizwa magonjwa hayo ambayo yanaweza kusababisha maumivu makali, ulemavu na athari nyinginezo mbaya.

Magonjwa ya kitropiki yaliyopuuzwa ni mjumuiko wa magonjwa 20 ambayo hutokea kwa kiasi kikubwa katika maeneo yenye hali ya hewa ya tropiki. Miongoni mwa magonjwa hayo ni wa matende na kuvimba miguu (Lymphatic filariasis au elephantiasis), Upofu wa mto (onchocerciasis au river blindness), kichocho (bilharzia, schistosomiasis), ugonjwa wa kulala ovyo (African trypanosomiasis) na maradhi mingine sugu ya ngozi n.k.

Fabian Ndenzako, kaimu mwakilishi wa WHO nchini Sudan Kusini amesema kuwa, wamejitolea kuisaidia Wizara ya Afya ya Sudan Kusini katika juhudi za kukabiliana na tishio la magonjwa ya tropiki yaliyosahaulika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live