Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WHO: Tutaendelea kugawa misaada ya kibinadamu katika eneo la Amhara Ethiopia

Migogoro Na Ukame Yasababisha Waethiopia Milioni Nne Kukosa Makazi   UN WHO: Tutaendelea kugawa misaada ya kibinadamu katika eneo la Amhara Ethiopia

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa litaendelea kutoa misaada ya kibinadamu katika eneo lililokumbwa na mgogoro mkubwa la Amhara nchini Ethiopia licha ya changamoto nyingi zinazotokana na ukosefu wa usalama.

Shirika hilo limesema hayo kwenye taarifa yake kwa kwa vyombo vya habari na kuongeza kuwa, WHO iinaendelea na juhudi zake za kuwafikishia misaada watu 95,000 wanaoishi katika mazingira magumu sasa ili kuhakikikisha kuwa wanaweza kupata mahitaji ya dharura ya kukabiliana na mambo mbalimbali yakiwemo maradhi ya kuambukiza kama kipindupindu, malaria na kuhudumia majeruhi wa vita.

Limesema, eneo la Amhara ambalo ni la pili kwa kuwa na watu wengi zaidi nchini Ethiopia linahitajia mno misaada ya dharura ya kiafya na kibinadamu tangu katikati ya mwaka huu wa 2023. Limesema hali hiyo imefanya utoaji wa vifaa kwa wahitaji kuwa kazi ngumu kwa timu ya WHO iliyoko katika eneo hilo. Hali ya wakimbizi huko Amhara Ethiopia, ni mbaya sana

Mbali na ukame, kipindupindu, malaria na miripuko ya surua, eneo la Amhara kwa sasa linakabiliwa na mzozo wa vita unaosababisha ongezeko la watu wanaouawa na kujeruhiiwa huku majeruhi wakikiimbilia kwenye vituo vya afya kutafuta huduma za afya, lakini vituo hivyo vya afya havina uwezo wa kuhudumia wimbi kubwa la watu.

Wiki iliyopita, WHO ilisema kuwa, karibu watu milioni 1.9 wamepatiwa chanjo ya kipindupindu licha ya mazingira yenye changamoto nyingi huko Amhara.

Migogoro ya kivita katika maeneo tofauti ya Ahmara hilo inasababisha pia kuongezeka idadi ya wakimbizi wa ndani (IDPs). Ukanda huo una zaidi ya wakimbizi 800,000 wa ndani, asilimia 12 kati yao wanaishi kwenye maeneo 40 yenye mrundikano wa watu.

Mwezi Agosti mwaka huu, Bunge la Ethiopia lilipasisha sheria ya kuongeza muda wa hali ya hatari kwa miezi sita huko Amhara huku mizozo ya muda mrefu kati ya wanajeshi na wanamgambo wa eneo hilo ikiendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live