Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WHO: Pombe chanzo ugonjwa wa kisukari Afrika

Kisukari 640x400 WHO: Pombe chanzo ugonjwa wa kisukari Afrika

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa, ugonjwa wa kisukari unaathiri idadi kubwa ya watu barani Afrika kutokana na ukuaji wa haraka wa miji, mtindo mbovu wa maisha kama wa kukaa chini sana, utaratibu mbovu wa kula chakula pamoja na unywaji wa pombe na ulevi.

Shirika hilo lilitoa taarifa yake hiyo jana Jumanne ambayo ilikuwa ni Siku ya Kisukari Duniani. Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika, alisema, bara hilo lina watu wazima milioni 24 wanaoishi na kisukari, na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka hadi milioni 55 ifikapo mwaka 2045.

Amesema, ugonjwa wa kisukari ulisababisha vifo vya watu 416,000 barani Afrika mwaka 2021 na inakadiriwa kwamba utakuwa moja ya sababu kuu za vifo barani Afrika ifikapo mwaka 2030, kama jamii za watu wa bara hilo hawatobadilisha mtindo wao wa maisha. Diabets, ugonjwa wa kisukari ni tishio barani Afrika na duniani

Aidha amesema, ugonjwa wa kisukari unasababisha matatizo ya kiuchumi kwa familia, akisisitiza kuwa, uchunguzi wa mara kwa mara pamoja na matibabu bora ni muhimu katika kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.

Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika pia amesema, asilimia 54 ya watu wanaoishi na kisukari barani Afrika hawajua kuwa wana ugonjwa huo. Na wengine wengi hawajua kuwa wako katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa huo kutokana na kutopima afya zao.

Vile vile amezitaka serikali za nchi za Afrika kuwekeza katika jitihada za kuzuia ugonjwa wa kisukari ikiwa ni pamoja na kubadilisha mtindo wa maisha ya watu, utaratibu mbovu wa ulaji chakula, kupunguza unywaji pombe, kuhimiza watu kufanya mazoezi na kutoa dawa za kuokoa maisha kwa wagonjwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live