Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WFP yasitisha usambazaji wa chakula Tigray, Ethiopia

WFP Yasitisha Usambazaji Wa Chakula Tigray, Ethiopia WFP yasitisha usambazaji wa chakula Tigray, Ethiopia

Tue, 2 May 2023 Chanzo: Voa

Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya chakula limesitisha kusambaza misaada katika mkoa wa kaskazini wa Ethiopia, Tigray.

Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya chakula limesitisha kusambaza misaada katika mkoa wa kaskazini wa Ethiopia, Tigray.

Hatua hiyo imefanyika ikiwa ni katikati ya uchunguzi kuhusu wizi wa chakula ambacho kilipaswa kupewa watu wenye njaa kwa mujibu wa wafanyakazi wanne wa misaada.

Mpango huo wa chakula duniani (WFP) unahusika na kusambaza chakula kutoka Umoja wa Mataifa na washirika wengine kwenda Tigray katikati mwa vita vya miaka miwili vya wenyewe kwa wenyewe vilivyo malizika kwa makubaliano ya kusitisha mapigano mwezi Novemba.

Zaidi ya watu milioni 5 wa eneo hilo lenye watu milioni 6 wanategemea misaada.

Mwezi uliopita shirika la habari la AP liliripoti kwamba WFP ilikuwa inachunguza madai ya matumizi mabaya ya chakula na kupelekwa kusiko stahiki nchini Ethiopia, ambapo watu milioni 20 wanahitahi misaada ya kibinadamu kutokana na ukame na mgogoro.

WFP iliwasiliana na washirika wake wa kimisaada Aprili 20 na kuwaeleza kwamba inasimamisha usambazaji wa chakula mkoani Tigray, mmoja wa wafanyakazi wa utoaji misaada aliliambia shirika la habari la AP.

Chanzo: Voa