Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WFP yasitisha msaada wa chakula kwa mji wa Sudan uliotekwa

WFP Yasitisha Msaada Wa Chakula Kwa Mji Wa Sudan Uliotekwa WFP yasitisha msaada wa chakula kwa mji wa Sudan uliotekwa

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa limesitisha kwa muda msaada wa chakula katika baadhi ya maeneo ya jimbo la kati la Gezira nchini Sudan, siku chache baada ya Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kuudhibiti mji wa Wad Madani katika jimbo hilo.

"Sehemu ya kimbilio sasa imekuwa uwanja wa vita katika vita ambavyo tayari vimewaathiri vibaya raia," mkuu wa Shirika la Chakula wa Umoja wa Mataifa (WFP) nchini Sudan, Eddie Rowe, alisema katika taarifa yake Jumatano.

"Hii imewalazimu WFP kusimamisha utoaji wa chakula katika baadhi ya maeneo katika jimbo la Gezira wakati ambapo watu wanahitaji msaada wetu zaidi."

Takriban watu 300,000 wamekimbia mapigano katika jimbo hilo tangu Ijumaa wiki jana, shirika hilo lilisema.

WFP imekuwa ikitoa msaada wa chakula kwa watu 800,000 huko Gezira na wale waliokimbia makazi yao kutokana na mzozo katika mji mkuu wa Sudan Khartoum.

Kuna wasiwasi kwamba kuenea kwa mapigano huko Gezira kunaweza kuzidisha mzozo wa kibinadamu wa Sudan.

Article share tools

Chanzo: Bbc