Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WFP wadai kuvamiwa na kuporwa shehena ya vyakula Sudan

WFP EWthiooo WFP wadai kuvamiwa na kuporwa shehena ya vyakula Sudan

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Sudan, shirika mpango wa chakula duniani WFP, limesema kuwa watu wasiojulikana walivamia msafara wake jumapili iliopita na kupora shehena ya misaada ya chakula iliokusudiwa kuwasadia maelfu ya raia katika eneo la Darfur ya kati.

Kupitia ukurasa wake wa X, mratibu wa misaada nchini Sudan, Clementine Nkweta-Salami, ameelezea kusikitishwa na tukio hilo, wakati WFP nayo ikizitaka mamlaka kuhakikisha wahusika wanawajibishwa.

Aidha WFP pia imesisitiza umuhimu wa mamlaka za nchi hiyo kuhakikisha njia salama ya kufikisha misaada kwa raia wanaohitaji.

Tukio hili la uporaji linakuja wakati huu hali ya kibinadamu ikiripotiwa kuendelea kuwa mbaya kutokanana vita vinavyoendelea kati ya jeshi ya wapiganaji wa RSF na kuiweka taifa hilo kwenye hatari ya kukumbwa na njaa kali.

Kwa mujibu wa takwimu, zaidi ya nusu ya raia wa Sudan ambao ni sawa na watu milioni 26 wako katika hatari ya kukumbwana viwango vya juu vya njaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live