Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WFP inahitaji dola milioni 351 kuimarisha misaada Somalia

EU Yasitisha Msaada Wa Chakula Kwa Somalia WFP inahitaji dola milioni 351 kuimarisha misaada yake nchini Somalia

Sun, 29 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetangaza kuwa, linahitaji dola za Kimarekani milioni 351 katika ufadhili jumla kwenye shughuli zote ili kuongeza msaada wa kibinadamu kwa miezi sita ijayo nchini Somalia.

Madhara ya miongo kadhaa ya migogoro ya silaha, mvua zisizo za kawaida, umaskini na wakimbizi wa ndani vimesababisha mamilioni ya watu nchini Somalia kuelekea kwenye njaa kali na uhaba wa chakula.

Kwa mujibu wa shirika hilo la Umoja wa Mataifa, kati ya Oktoba na Desemba, takriban watu milioni 4.3 watakuwa wanakabiliwa na mgogoro mbaya zaidi wa uhaba wa chakula, huku milioni moja wakihitajia misaada ya dharura ya kukabiliana na baa la njaa.

Katika ripoti yake ya hivi karibuni kabisa, WFP imesema kwamba, idadi ya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wanaokadiriwa kukabiliwa na utapiamlo mkali mwaka 2023 imepungua hadi milioni 1.5, huku watoto 331,000 wakiwa bado wanakabiliwa na utapiamlo unaotishia maisha.

Mbali na majanga mengineyo, Somalia inakumbwa mara kwa mara na majanga mengine kama ya nzige

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, takriban watu milioni 1.2 wanaoishi katika maeneo ya vijijini, mijini na wakimbizi wa ndani kwenye maeneo ya mafuriko wanakabiliwa na vitisho vya mafuriko kutokana na athari ya pamoja ya El Nino na hali nzuri ya Bahari ya Hindi wakati wa msimu wa mvua wa Deyr unaoanzia mwezi Oktoba hadi Desemba.

Ripoti hiyo imeonya kwamba, mafuriko ya ghafla yanayotarajiwa katika maeneo ya mijini yanaweza kuathiri watu wengi, kwani zaidi ya nusu ya makazi ya watu katika maeneo ya tambarare yanayokumbwa na mafuriko.

Kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) la Umoja wa Mataifa, karibu Wasomali milioni 1.2 wanaweza kuathiriwa na mafuriko katika muda wa miezi mitatu ijayo.

WFP imetangaza pia kwamba, hatua za kutarajia kufuatia kuanza mafuriko yanayotarajiwa yatalenga kusaidia watu katika maeneo yaliyoko hatarini kukumbwa na mafuriko katika mikoa ya Hiraan, Shabelle ya Kati, Gedo na Shabelle ya Chini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live