Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WFP: Watu milioni 1.4 hatarini kukumbwa na njaa Chad

Chad Chakula Wfp WFP: Watu milioni 1.4 hatarini kukumbwa na njaa Chad

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeonya kuhusu uwezekano wa kusitishwa msaada wake wa chakula na lishe kwa watu milioni 1.4 walioathiriwa na mgogoro nchini Chad - ikiwa ni pamoja na wakimbizi wapya wa Sudan - kutokana na vikwazo vya fedha.

Haya yanajiri wakati mashirika ya misaada yakihangaika kujibu wimbi jipya la wakimbizi wanaokimbia janga la kibinadamu lisilofikirika linalotokea katika jimbo jirani la Darfur nchini Sudan huku kukiwa na ripoti za mauaji ya watu wengi, ubakaji na uharibifu mkubwa.

Pierre Honnorat, Mkurugenzi wa WFP nchini Chad, Jumanne akiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, N'djamena, nchini Chad, alionya kwamba, katika kipindi cha miezi sita tu ya vita nchini Sudan, wakimbizi wengi wamekimbilia Chad kama walivyovuka hadi katika miaka 20 iliyopita kuanzia kuzuka kwa mgogoro wa Darfur mwaka wa 2003. Amesema jumla ya idadi ya wakimbizi nchini Chad hivi sasa ni zaidi ya milioni moja, na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa mwenyeji wa mojawapo ya idadi kubwa ya wakimbizi wanaokuwa kwa kasi zaidi katika bara zima la Afrika.

Aidha amesema, mgogoro wa Chad umesahaulika kwani macho ya ulimwengu yako kwenye dharura zingine, na kuongeza kwamba: "Inashangaza lakini watu wengi wa Darfur wamekimbilia Chad katika kipindi cha miezi sita iliyopita kuliko miaka 20 iliyopita."

Afisa huyo wa WFP amebaini kuwa kupunguza usaidizi wetu si chaguo kwa sababu itakuwa na matokeo yasiyoelezeka kwa mamilioni ya watu, na kuhatarisha miaka ya uwekezaji katika kupambana na njaa na utapiamlo nchini kutokana na uhaba wa fedha. Kuanzia Januari kusimamishwa huku kutaongezwa hadi kwa watu milioni 1.4 kote Chad, ikiwa ni pamoja na wakimbizi wapya waliowasili kutoka Sudan ambao hawatapokea chakula wanapokimbia kuvuka mpaka.

Zaidi ya hayo, Honnorat ameendelea kusema kuwa kupungua kwa ufadhili na kuongezeka kwa mahitaji ya kibinadamu kunalazimisha WFP kufanya maamuzi nagumu. Mwezi Disemba, WFP italazimika kusitisha msaada kwa wakimbizi wa ndani na wakimbizi kutoka Nigeria, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Cameroon

Chanzo: www.tanzaniaweb.live