Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WFP: Wakimbizi barani Afrika wanakabiliwa na uhaba wa chakula

WFP Wakimbizi Wakimbizi barani Afrika wanakabiliwa na uhaba wa chakula

Mon, 20 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeonya kwamba wanaotafuta hifadhi katika nchi za Afrika Mashariki na Magharibi wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na uhaba wa bajeti.

Kwa mujibu wa taarifa, robo tatu ya waomba hifadhi wanaofadhiliwa na shirika hilo katika Afrika Mashariki wamepoteza asilimia 50 ya mgao wao wa chakula, huku wakimbizi walio Ethiopia, Kenya, Sudan Kusini na Uganda wakiteseka zaidi.

"Tunapaswa kufanya uamuzi wa kuhuzunisha ili kupunguza mgao wa chakula wanaotafuta hifadhi ambao wanatutegemea kwa ajili ya maisha yao," David Beasley, mkurugenzi mtendaji wa Mpango wa Chakula Duniani amesema.

Beasley ameongeza kuwa bajeti iliyopo haiendani na kuongezeka kwa mahitaji ya chakula duniani. Katika eneo la Afrika Maghaŕibi – hasa katika Burkina Faso, Cameroon, Chad, Mali, Mauritania na Nigeŕ – Mpango wa Chakula Ulimwenguni umepunguza kwa kiasi kikubwa chakula kinachowafikia wakimbizi.

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa ameonya kwamba upungufu wa chakula unakaribia nchini Angola, Malawi, Msumbiji, Kongo, Tanzania na Zimbabwe.

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani lilitangaza wiki iliyopita kuwa linahitaji dola milioni 426 katika kipindi cha miezi sita ijayo ili kuzuia njaa nchini Sudan Kusini, ambako zaidi ya theluthi mbili ya watu wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Takriban watu milioni 8.3 wakiwemo wanaotafuta hifadhi wanatarajiwa kukabiliwa na njaa kali nchini Sudan Kusini mwaka huu.

Vita vya Ukraine vimezidisha kwa kiasi kikubwa mzozo wa wakimbizi duniani na hatari ya njaa na pia kupandisha bei ya bidhaa, hasa nafaka.

Siku ya Ijumaa Rais Vladimir Putin wa Russia alisema ukoloni mamboleo ndio umesababisha migogoro ya kibinadamu inayoshuhudiwa katika sehemu mbalimbali duniani; na kwamba Marekani na nchi za Ulaya ndizo zinazopaswa kubebeshwa dhima iwapo dunia itatumbukia kwenye baa la njaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live