Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WFP: Programu za chakula shuleni ni daraja la mafanikio kwa wanafunzi maskini

Msosi Baadhi ya wanufaika na mradi wa chakula mashuleni

Tue, 12 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani (WFP) limesema afya na lishe bora vinaruhusu watoto kujifunza na kufanya vyema katika masomo yao na hivyo kupanua wigo wa fursa zao za kielimu.

Kwa mujibu wa WFP, lishe duni na kukosa mlo ni sababu kwa watoto wengi kutohudhuria masomo hasa katika nchi masikini zinazoendelea ikiwemo barani Afrika.

Mwezi uliopita wa Machi 2022 lilizindua kampeni kabambe ya kuchagiza programu za mlo mashuleni.

Kampeni hiyo pamoja na kusaidia watoto wote wenye uhitaji zimewawezesha watoto wa kike kusalia shuleni badala ya wazazi wao kuwaozesha mapema kutokana na ugumu wa maisha hali ambayo inakatiza ndoto zao za elimu na kuchangia katika mimba za utotoni.

WFP: Programu za chakula shuleni ni daraja la mafanikio kwa wanafunzi maskini Mwandishi Wetu 0754Hrs   Aprili 12, 2022 Habari Humpa kila mtoto matumaini ya kujifunzia na motisha ya kusalia shuleni. Huzalisha kipato kwa wakulima wadogo kwa vyakula wanavyouza shuleni. Dar es Salaam. Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani (WFP) limesema afya na lishe bora vinaruhusu watoto kujifunza na kufanya vyema katika masomo yao na hivyo kupanua wigo wa fursa zao za kielimu.

Kwa mujibu wa WFP, lishe duni na kukosa mlo ni sababu kwa watoto wengi kutohudhuria masomo hasa katika nchi masikini zinazoendelea ikiwemo barani Afrika.

Mwezi uliopita wa Machi 2022 lilizindua kampeni kabambe ya kuchagiza programu za mlo mashuleni.

Kampeni hiyo pamoja na kusaidia watoto wote wenye uhitaji zimewawezesha watoto wa kike kusalia shuleni badala ya wazazi wao kuwaozesha mapema kutokana na ugumu wa maisha hali ambayo inakatiza ndoto zao za elimu na kuchangia katika mimba za utotoni.

Zinazohusiana

Twaweza: Wazazi wengi hawajui matokeo halisi ya shule za watoto wao Sababu za wazazi kuwaongoza watoto kusoma vitabu WFP imesema kuwa programu za mlo shuleni hutumika kama motisha kwa familia kuandikisha na kuwaweka watoto wao shuleni. Pia program hizo zinawapunguzia wazazi mzigo wa kupanga bajeti ya chakula cha mchana, huwaongezea mapato na kusaidia kupunguza umaskini.

Kwa mujibu wa WFP, milo ya shuleni inawakilisha asilimia 10 ya mapato ya kaya maskini na zilizo hatarini, na hiyo ni akiba kubwa kwa familia zilizo na mtoto zaidi ya mmoja.

Katika kunufaisha watoto na familia zao, WFP imesema mlo shuleni na afya husaidia kujenga “mtaji wa kibinadamu” ambao inajumuisha afya ya watu, ujuzi, elimu, uzoefu na mazoea.

WFP imesema thamani ya programu za mlo shuleni ni kubwa zaidi ya mlo mmoja. Na kupitia shirika hilo sasa programu hizo zinawafikia watoto wa shule milioni 15 katika nchi 61.

Juhudi hizo humpa kila mtoto matumaini ya kujifunzia na motisha ya kusalia shuleni huku zikizalisha kipato kwa wakulima wadogo kwa vyakula vinavyonunuliwa na WFP ndani ya nchi kwa ajili ya kulisha watoto hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live