Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vyuo vikuu 30 Morocco vyaungana na Palestina

Vyuo Vikuu 30 Vya Morocco Vyuo vikuu 30 Morocco vyaungana na Palestina

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanachuo wa vyuo vikuu mbalimbali vya Morocco wametangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina hususan mashahidi wa Gaza.

Zaidi ya vyuo vikuu 30 vya Morocco vilifungwa na kutoendesha shughuli za masomo kwa ajili ya kutangaza himaya, uungaji mkono na mshikamano na watu wa Palestina hususan mashahidi wa Ukanda wa Gaza.

Muungano wa Taifa wa Wanafunzi wa Morocco sambamba na kutoa taarifa umetangaza kwamba wanafunzi na wahadhiri wa vyuo vikuu 32 vya nchi hiyo pamoja na vyuo vikuu vya Agadir katikati na Rabat kaskazini mwa nchi, wakati wa kuandaa maandamano, walifunga vyuo kwa siku moja kulaani mauaji ya watu katika Hospitali ya al-Ma'madani huko Gaza na Mauaji Mengine ya Israel na kueleza kwamba, hujuma hiyo yay Israel ni "jinai za kivita".

Kwa upande mwingine, ofisi ya rais wa Algeria pia imelaani kile ilichokiita "mashambulizi ya makusudi ya vikosi vinavyoikalia kwa mabavu Palestina dhidi ya hospitali ya Gaza".

Ropoti kutoka maeneo mbalimbali ya dunia, zinaonyesha kuwa, maandamano yameendelea kushuhudiwa katika nchi mbalimbali kulaani mauaji ya makusudi ya Israel dhidi ya Hospitali ya al-Ma'madani ambayo ndani yake kulikuweko wagonjwa na majeruhi waliokuwa wameomba hifadhi hapo. Maandamano ya wananchi wa Morocco dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel

Wakati huo huo, shirika moja la kutetea haki za binadamu lenye makao yake mjini Geneva Uswisi limesema kwa wastani utawala haramu wa Israel unaua shahidi watoto 100 wa Kipalestina katika kila saa 24 katika Ukanda wa Gaza.

Shirika la Euro-Mediterranean Human Rights Observatory lenye makao yake mjini Geneva limeongeza kuwa, watoto ndio wahanga na walengwa wa kwanza wa 'umwagaji damu' unaoendelea dhidi ya Wapalestina Gaza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live