Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vyuo Vikuu Nigeria kufungwa kupisha Uchaguzi

Unilag Best Universities In Nigeria Vyuo Vikuu Nigeria kufungwa kupisha Uchaguzi

Fri, 10 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya Taifa ya Vyuo Vikuu nchini Nigeria (NUC),imeamuru Vyuo Vikuu nchini humo kufungwa kuanzia Februari 22 mpaka Machi 14 kutokana na Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Februari 25.

Uamuzi huo umetokana na wasiwasi juu ya Ulinzi na Usalama wa wafanyakazi na wanafunzi katika kipindi cha uchaguzi.

Taarifa kutoka kwenye Vyombo vya habari vya Nigeria zinaeleza kuwa amri hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu wa nchi hiyo Bw.Adamu Adamu.

Kumekuwa na wasiwasi juu ya uwezekano wa uchaguzi huo kuendelea kama ulivyopangwa kutokana na matatizo ya Usalama nchini humo,hata hivyo Mkuu wa Tume ya Uchaguzi amesisitiza kuwa uchaguzi utafanyika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live