Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vurugu zaibuka kanisani, waumini wamkataa mchungaji mpya

ZADL1a01.jpeg Vurugu zaibuka kanisani, waumini wamkataa mchungaji mpya

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tafaruku zimetokea katika Kanisa la Kamtonga Africa Inland Church (AIC) eneo la Mwatate, Kaunti ya Taita Taveta nchini Kenya siku ya Jumapili baada ya waumini na uongozi wa eneo hilo kutofautiana kuhusu kusimikwa kwa mchungaji mpya.

Ibada ya Jumapili ilimalizika kwa mtafaruku baada ya baadhi ya waumini wa kanisa hilo kutaka kujua ni kwanini mchungaji mpya ameletwa kanisani bila kuzingatia maoni ya waumini.

Mchungaji Julius Kiendi alibadilishwa Jumapili na Mchungaji Alfred Muilu ambapo Mchungaji Kiendi wakati akiwaaga waumini amedai alitengwa na Baraza la Kanisa la Wilaya (RCC) wakati wa ibada ya makabidhiano.

“Tangu jana (viongozi wa kanisa) hawajaniruhusu kushiriki shughuli hii, baadhi ya viongozi wa kanisa hawakufurahi kwa sababu niliwaeleza dhambi zao,” amedai.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live