Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vurugu Kenya: Barabara ya Express yafungwa

Barabara Yafungwa Kenya Vurugu Kenya: Barabara ya Express yafungwa

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: Radio Jambo

Opereta wa Nairobi Expressway mnamo Jumatano, Julai 12, alifunga kwa muda sehemu za barabara ya Express way baada ya waandamanaji wanaopinga serikali kuharibu baadhi ya sehemu.

Opereta, Moja Expressway, ilitangaza kuwa walisimamisha huduma katika vituo vya Mlolongo, Syokimau na Standard Gauge Railway (SGR) kutokana na maandamano hayo.

Katika taarifa, mwendeshaji huyo alihakikisha kwamba wanajitahidi kurejesha hali ya kawaida hata kama maandamano dhidi ya kupanda kwa gharama ya maisha yakishika kasi.

Wenye magari katika barabara kuu wameshauriwa kutumia barabara ya JKIA.

Dakika chache mapema, waandamanaji waliharibu kizuizi na vituo vya utozaji ushuru karibu na Mlolongo, Kaunti ya Machakos.

Zaidi ya hayo, usafiri huo ulilemazwa baada ya vijana hao waliokuwa na ghasia kuwasha matairi kando ya barabara ya mwendokasi

Kwenye video zilizoonekana na Radiojambo waandamanji wanaonekana wakiwa na ghadhabu huku wakibomoa sehemu ya barabara ya Express Way Mlolongo kaunti ya Machakos.

Hata hivyo IG Koome alisema kuwa maandamano ambayo yaliitishwa na muungano wa Azimio sio halali.

Chanzo: Radio Jambo