Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viwango vya joto Kenya kupanda

Viwango Vya Joto Kenya Kupanda Viwango vya joto Kenya kupanda

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya Kenya imewataka Wakenya kujiandaa kukabiliana na halijoto ya juu wakati wa mchana katika maeneo mengi ya nchi kuanzia Jumanne.

Utabiri wa Februari 20 hadi Februari 26 unatabiri viwango vya juu vya joto la zaidi ya 30°C katika kaunti za Turkana, Samburu, Marsabit, Mandera, Wajir, Isiolo, Garissa na Tana River.

Lamu, Kilifi, Mombasa, Kwale, Taita Taveta, Kajiado, Makueni, Kitui, Machakos, Nairobi, Kiambu, Embu, Laikipia na Baringo pia zitaona wastani wa halijoto ya juu zaidi ya 30°C.

Ni sehemu tu za Meru, Tharaka Nithi, Murang’a, Nyeri, Nyandarua, Nakuru, Elegeyo Marakwet, Trans Nzoia na Pokot Magharibi ndizo zinazotarajiwa kupata wastani wa viwango vya chini ya vya nyuzi joto 25°C.

Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) wiki iliyopita lilitangaza kuwa dunia ilikuwa na joto zaidi mwezi Januari kuwahi kurekodiwa mwaka huu.

Chanzo: Bbc