Tofauti na Yesu Kristo ambaye tunasikia kuhusu habari zake, Kaunti ya Bungoma nchini Kenya, kuna Yesu wa Tongaren ambaye mwishoni mwa wiki ameibua shutuma dhidi ya waumini wake ambao wamepanga kumsulubisha siku ya Ijumaa Kuu ya Pasaka na kukimbilia polisi kuomba msaada kuokoa maisha yake. Mwishoni mwa wiki aliibua gumzo kwenye mitandao ya jamii baada ya kusambaa taarifa akiwashutumu waumini wake kuwa wana njama za kumtoa uhai kwa kile alichoeleza kuwa wanataka kumsulubisha msalabani itakapojiri Ijumaa Kuu kabla ya Pasaka. Kiongozi huyo wa kiroho, anayefahamika kwa jina halisi Eliud Simiyu anaongoza Kanisa la New Jerusalem ambaye pia ni baba wa watoto 7 alifikia hatua ya kwenda kujisalimisha polisi na kunukuliwa kwamba “Sikubaliana na hatua ya waumini kutaka kunisulubisha msalabani”.
Waumini wanawake Kanisa lake lina idadi kubwa ya wanawake ambao huwa hawaruhusiwi kukata nywele. Eliud kama anavyojulikana na wafuasi wake ‘yesu wa Tongaren’ ambao wengi ni wanawake, humzunguka na kumsujudia jambo ambalo anachukulia ni malaika. Waumini wake wanatakiwa kuchagua majina ya malaika na manabii mbalimbali. Ndiyo sababu hata yeye alichagua jina hilo ambalo baada ya kuanza huduma.
Pasaka yake ni Julai Mwaka 2019' yesu wa Tongaren, Kaunti ya Bungoma aliahidi kutosulubishwa kabla ya Pasaka yake itakayosherehekewa Julai 2018. Wakati wa mahojiano na BBC Swahili, Eliud Simiyu alisema kulingana na mafunzo ya kanisa lake, Pasaka katika kanisa lake, “New Jerusalem” itasherehekewa katikati mwa Julai. Hata hivyo, kiongozi huyo haamini katika kusulubishwa kwa Yesu kama Biblia inavyosema ambapo inaelezwa ndipo msingi wa imani ya Wakristo wengi wanayoamini na kufuata.
Kuongeza vitabu vya Biblia Kulingana na mtazamo wake anadai kwamba, Biblia ya Agano la Kale na Agano Jipya ambayo hutumiwa ulimwenguni haijakamilika na kuna haja ya kuongeza vitabu zaidi. "Nitaongeza vitabu vya Mbingu Mpya na Nchi Mpya vitakavyochapishwa ili kukamilisha Agano Jipya na Agano la Kale,” alinukuliwa kiongozi huyo.
Historia ya kujipachika majina Historia ya eneo hilo inaonyesha siyo kiongozi huyo wa kwanza kujiita Yesu katika Kaunti ya Bungoma. Awali, kulitokea mwanamume mmoja aliyejiita kama "Jehova Wanyonyi. Si mara ya kwanza kwa eneo hilo la magharibi mwa kwa Kenya kujitambulisha mtu kuwa anauwezo wa kuaminiwa kiimani.
Katika miaka ya nyuma, Jehova Wanyonyi alidai kuwa yeye ndiye Mungu. Alikuwa ameoa wanawake zaidi ya wanawake 10 na watoto zaidi ya 100. Wake zake pamoja na watu wengine watano waliomzingira wakati wote walijiita malaika.