Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita ya Sudan inaweza kuingiza ukanda mzima katika janga - UN

Mzozo Wa Sudan: Mapigano Yachacha Karibu Na Ngome Ya Jeshi Vita ya Sudan inaweza kuingiza ukanda mzima katika janga - UN

Fri, 25 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Umoja wa Mataifa unasema vita nchini Sudan vina madhara makubwa kwa nchi nzima na vinaweza kuliingiza eneo lote katika janga la kibinadamu.

Mapigano kati ya jeshi na jeshi la wanamgambo yalianza mnamo Aprili na yanaenea. Umoja wa Mataifa unasema mamia kwa maelfu ya watoto wana utapiamlo uliokithiri na wako katika hatari ya kifo ikiwa hawatatibiwa.

Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa anasema njaa, magonjwa na watu kuyahama makazi yao vinatishia kuiangamiza kabisa Sudan.

Kumekuwa na ripoti nyingi za kutisha kuhusu athari za vita hivyo lakini Martin Griffiths anapendekeza kwamba ikiwa mapigano kati ya jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka yataendelea, eneo lote litakabiliwa na matokeo mabaya.

Wiki hii shirika la usaidizi la Save The Children lilisema kwa sababu ya ghasia limelazimika kufunga makumi ya vituo vyake vya lishe. Ilisema zaidi ya watoto 30,000 walikosa matibabu na matokeo yake ni karibu 500 walikufa.

Chanzo: Bbc