Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita vya Tigray vimeua watu 600,000 - Mpatanishi wa AU

Trigayyyy Vita vya Tigray vimeua watu 600,000 - Mpatanishi wa AU

Mon, 16 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mpatanishi wa Umoja wa Afrika katika mzozo wa Tigray nchini Ethiopia, Olusegun Obasanjo, ameliambia gazeti la Financial Times (FT) kwamba watu wapatao 600,000 wanaweza kuwa wamekufa katika vita hivyo vya miaka miwili.

Katika mahojiano na jarida hilo, Bw Obasanjo alisema idadi ya waliofariki ilikuwa "takriban 600,000".

Licha ya kwamba idadi ya watu waliofariki katika mzozo huo ni vigumu kuthibitisha.

Watafiti hapo awali wamekadiria vifo hivyo hadi mamia ya maelfu.

Siku ya Jumapili, FT ilimnukuu mkuu wa tume ya haki za binadamu wa Ethiopia, Daniel Bekele, akisema kwamba makadirio yaliyotolewa na pande zote yanahitaji kuchukuliwa kwa tahadhari kwani haiwezekani "kujua idadi kamili ya waliopoteza maisha".

Mzozo huo ulianza Novemba 2020, wakati Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alipoamuru mashambulizi ya kijeshi dhidi ya vikosi vya eneo hilo huko Tigray - ambapo alisema ilikuwa jibu kwa shambulio la kambi ya kijeshi inayohifadhi wanajeshi wa serikali.

Ingawa Novemba mwaka jana serikali ya Ethiopia na waasi wa Tigray walitia saini ya makubaliano ya kusitisha vita hivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live