Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita vya Sudan: Watu 200 wafariki dunia

Vita Vya Sudan: Watu 200 Wafariki Dunia Vita vya Sudan: Watu 200 wafariki dunia

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: Voa

Mapigano kati ya jeshi na wanamgambo nchini Sudan yamesababisha vifo vya takriban watu 200 na kujeruhi 1,800, kuharibu mahospitali na kukwamisha misaada siku ya Jumatatu kufuatia mapigano ya siku tatu katika vita hivyo vinavyopiganwa mjini.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alizitaka pande zinazopigana nchini Sudan kusitisha uhasama mara moja huku msafara wake ulielekea mjini Khartoum.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alisema ongezeko la mzozo kati ya jeshi na makundi ya kijeshi, wakiongozwa na majenerali wapinzani, "unaweza kuleta athari kubwa nchini humo na katika eneo la kanda hiyo."

Vurugu hizo ambazo zilizuka siku ya Jumamosi, zimekuwa zikiendelea kwa muda wa siku ya tatu hadi Jumatatu, huku idadi ya vifo vya watu vikiongezeka hadi kufikia vifo wasiopungua 185, Volker Perthes, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, aliwaambia waandishi wa habari.

Mapigano hayo yalizuka kufuatia wiki kadhaa za vita vya kugombania madaraka kati ya majenerali wawili walionyakua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka 2021: Mkuu wa jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, na makamu wake, Mohamed Hamdan Daglo, ambaye ni kamanda anayeongoza kikosi cha Rapid ambacho ni kikosi cha kijeshi chenye nguvu. Umoja wa Mataifa umesitisha shughuli zake nyingi nchini humo, alisema msemaji wa Guterres, Stephane Dujarric, ambaye alisisitiza Umoja wa Mataifa "hautawataka wafanyikazi kwenda kazini wakati ni wazi kwamba usalama wao hauna uhakika."

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya mkutano wa faragha kuhusu hali ilivyo nchini Sudan Jumatatu asubuhi.

Wanachama watatu wa baraza la nchi za Afrika lenye wanachama 15 -- Ghana, Gabon na Msumbiji -- walitoa taarifa ya pamoja kufuatia mkutano huo, wakitaka "kusitishwa kwa mapigano mara moja."

Chanzo: Voa