Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita Sudan: Watu 715 hawajulikani walipo

Miezi 5 Ya Mzozo Sudan Yasababisha Adha Kubwa Kwa Watoto Katika Kambi Vita Sudan: Watu 715 hawajulikani walipo

Sun, 22 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi moja la haki za binadamu la Sudan limesema kuwa, watu 715 wametoweka na hakuna rekodi zao zoaote kutokana na mgogoro wa vita unaoendelea baina ya majenerali wa kijeshi nchini humo.

Kundi la SGVED linaloshushulikia wahanga waliotoweka kwa lazima kwenye mgogoro wa Sudan limesema kwenye ripoti yake hiyo ya jana Jumamosi kwamba: "Raia 715 wametoweka nchini Sudan katika kipindi hiki cha miezi sita ya vita kati ya jeshi la nchi hiyo (SAF) na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF)."

Ripoti hiyo imefuatilia ukiukaji wa haki za binadamu pamoja na utekaji nyara, kuwekwa kizuizini na kutoweka watu kiholela tangu Aprili 15 vilipoanza vita hivyo hadi Oktoba 15, na inajumuisha mji mkuu Khartoum na miji mingine ya Sudan.

Katika ripoti yake hiyo, kundi hilo limesema, kati ya watu hao waliotoweka kwa lazima, wanaume ni 666, huku 650 kati yao wakiwa watu wazima na 16 ni watoto 16 wanaume. Kati ya watu hao wanawake ni 49, ambapo 47 ni watu wazima na 2 watoto wadogo wa kike.

Vita baina ya majenerali wa kijeshi vinaendelea kufanya uharibifu mkubwa nchini Sudan

Mji wa Khartoum una rekodi ya idadi kubwa zaidi ya kesi 309 za watu walitoweka kilazima, huku 156 wakiwa ni wa mji wa Omdurman, 130 wametoweka huko Bahri, na kesi wengine wametoweka katika majimbo ya Kordofan Kaskazini, Jimbo la Darfur Kusini, Darfur Kaskazini, Jimbo la Darfur Magharibi na Jimbo la Darfur ya Kati.

Sudan imekumbwa na mapigano makali kati ya majenerali wa kijeshi wa SAF na RSF tangu tarehe 15 Aprili mwaka huu na kusababisha watu wasiopungua 3,000 kuuawa na zaidi ya 6,000 kujeruhiwa, kama zinavyoonesha takwimu za Wizara ya Afya ya Sudan.

Kwa mujibu wa Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM), karibu watu milioni 5.8 wamekimbia makazi yao ndani na nje ya Sudan kutokana na vita hivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live