Takriban wahamiaji 1,500 wa Kiafrika waliwasili kwenye ufuo wa Visiwa vya Canary wikendi hii, kulingana na idara ya huduma za dharura za visiwa hivyo vya Uhispania. Inakadiriwa kuwa tangu kuanza kwa mwaka 2023, wahamiaji wapatao 27,000 wametoka Afrika, hasa pwani ya Senegal. Idadi ya wahamiaji wanaowasili ni kubwa na kwamba kuna hatari ya idara ya huduma za dharura kuzidiwa.
Katika kisiwa cha Tenerife, zaidi ya wahamiaji 10,000, hasa Wasenegali, wametua tangu mwanzoni mwa mwezi wa Oktoba katika visiwa vya Canary, ambavyo vituo vyao vya mapokezi vimejaa kabisa, anasema mwandishi wetu huko Madrid, François Musseau. Kiasi kwamba wahamiaji wengi hawajaweza kupata mahali pa kulala. Kuna wengi wao ambao mamlaka ya Uhispania haiwapi tena wanasheria, hali ambayo inasababisha hali ngumu sana kwa mama wa familia au watoto ambao hawatambuliwi tena na ambao mahitaji yao hayawezi kufikiwa tena.
Mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali yanashutumu kushindwa vibaya kwa utawalawa sheria. Kuhusu mamlaka, wanakabiliwa na ukweli kwamba mamlaka ya Senegal haiheshimu tena mkataba unaoruhusu kuondolewa kwao. "Kinachotokea ni kwamba baada ya siku tatu katika kituo cha polisi, wanaachiliwa, ni wazi watoto wadogo wanatunzwa na serikali inayojitegemea ya Canary," anaelezea Laetitia Marthe wa Mtandao wa Mshikamano na Wahamiaji katikaCanary, akihojiwa na Claire Fages kutoka kitengo cha Afria cha RFI. Lakini watu wazima, wakishakaa katika vituo vya mapokezi kwa miezi michache, wana uhuru wa kutememba, kwa hiyo ni uhuru wa kinafiki kwa vile wapo katika hali isiyo ya kawaida, hivyo hawana haki ya kufanya kazi, hawawezi kuchukua ndege kwenda katka bara la Afrika wakati hakuna sababu ya kuzuia uhuru wa kutembea ndani ya nchi hiyo. "
Matokeo yake, wahamiaji hao wa Senegal, walioingia nchini Uhispania kwa sababu za kiuchumi na kwa sababu za kukosekana kwa utulivu wa kisiasa, wanaongezeka kwa idadi kila siku. Kufikia sasa, maelfu ya watu wamesafirishwa kwa ndege hadi kwenye rasi ya Uhispania, lakini tena, serikali inasema, hali inazidi kuwa ngumu kwa kuwatuma kwenye vituo vya mapokezi. Ukosefu wa wakalimani
Spitou Mendy, mkalimani wa shirika lisilo la kiserikali la Accem, huko Lanzarote, kisiwa katika visiwa vya Uhispania, anaelezea kwamba maneno ya kwanza anayopaswa kutafsiri, kutoka kwa Wolof au Dioula, mara nyingi ni magonjwa ya kimwili kutokana na kusafiri baharini: wanawake wanaowasiki wakiwa na majeraha ya moto kwa sababu baharini kuna mchanganyiko wa dizeli na maji ya chumvi, na hiyo si nzuri kwa ngozi. " Wakalimani basi ni muhimu kuwasaidia wahamiaji, ambao mara nyingi hukwama kutokana na kukosa vibali, kutatua hali zao za kiutawala. Hata hivyo, kama wanasheria, wakalimani ni wachache sana, miaka 30 baada ya kuwasili kwa mara ya kwanza kwa wahamiaji katika Canary.