Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Virusi vya corona ‘kupandisha bei’ za nguo, vifaa vya kielektroniki Kenya

Virusi vya corona ‘kupandisha bei’ za nguo, vifaa vya kielektroniki Kenya

Wed, 4 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Maduka makubwa ya rejareja nchini Kenya yanafikiria kupandisha bei za bidhaa kama nguo, samani, simu za mkononi, televisheni na majokofu kutokana na mlipuko wa virusi vipya vya corona kuathiri usafirishaji wa bidhaa duniani.

Maduka hayo, ambayo yalisafiriasha bidhaa kwa wingi kabla ya mwaka mpya wa Kichina mwezi Januari, yanasema kuwa bidhaa zitaanza kupungua baada ya wiki tatu.

Virusi hivyo vimeshaua watu takriban 3,000 nchini China na kusababisha kufungwa kwa viwanda katika nchi hiyo ya barani Asia, na kuumiza ugavi wa bidhaa duniani, ikiwemo Kenya ambayo ilinunua asilimia 20.2 ya mauzo ya bidhaa za nchi hiyo nje katika kipindi cha miezi 11 kinachoishia mwezi Novemba.

Kenya inaingiza bidhaa kadhaa kutoka China huku simu za mkononi zikiongoza. Bidhaa nyingine ni nguo, vifaa vya jikoni, samani, mashine na vifaa tiba.

Kutokana na hali hiyo, maduka hayo makubwa sasa yanatafuta nchi nyingine yanakoweza kuagiza bidhaa, yakisema uamuzi huo utasababisha wateja kulipia zaidi kwa kuwa masoko mbadala ni ghali kulinganisha na China.

“Tayari tuna tatizo na wanaosafirisha bidhaa, na athari zake zitakuwa bayana mwishoni mwa mwezi,” alisema ofisa mkuu wa biashara wa Naivas, Willy Kimani. “Tunategemea bei za bidhaa muhimu, hasa za kielektroniki, nguo na matoi zitapanda kwa sababu ya gharama za ugavi na ukweli kwamba tunazipata kutoka katika masoko ambayo ni ghali.”

Pia Soma

Advertisement

Naivas sasa imepanua wigo wake wa sehemu za kuagiza bidhaa ikijumuisha nchi za barani Ulaya, Uturuki na Brazil.

“Tumetaarifiwa na baadhi ya kampuni zinazotuuzia bidhaa kuwa kutakuwa na upungufu wa baadhi ya vitu,” alisema ofisa mtendaji mkuu wa Tuskys, Dan Githua alipoongea na Business Daily. “Tumekuwa tukitafuta pia sehemu mbadala za kuagiza bidhaa. Na tumebaini kuwa bei zitapanda.” Business Daily

Chanzo: mwananchi.co.tz