Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wawili ADF wauawa DRC

Adf C46d7b XL Viongozi wawili ADF wauawa DRC

Fri, 12 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majeshi ya Congo na Uganda yameripotiwa kuwaua waasi wa kundi la ADF Kaskazini mwa maeneo ya Beni.

Maafisa kutoka Majeshi mawili ya nchi hizo walitangaza kwamba hivi karibuni wamewaua wafuasi wawili wa kundi hilo, viongozi wanaojulika kwa jina la Daktari “Musa Baluku”, mnamo Aprili 8 na Kamanda “Baghdad”.

Viongozi hao Musa Baluku na Lumisa Mohammed walikuwa wanachukuliwa kama Viongozi wa mstari wa mbele wa Kiislamu nchini DRC ambapo wote wawili waliwekewa vikwazo na Marekani tangu 2019.

Kundi la ADF linalopinga Serikali ya Uganda, limekuwa likiendesha mashambulizi nchini DRC malengo ikiwa ni katika kutaka kufanya mapinduzi dhidi ya Rais Yoweri Museveni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live