Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi waliofanya mapinduzi wasamehewa

4aa5469f Cd84 4b15 93df Cfd30c4e34b3.jpeg Viongozi waliofanya mapinduzi wasamehewa

Fri, 17 Sep 2021 Chanzo: millardayo.com

Viongozi waliofanya mapinduzi mawili ya hivi karibuni nchini Mali wamepewa msamaha na bunge la mpito la nchi hiyo.

Kanali Assimi Goïta na waaafisa wengine wa kijeshi waliohusika katika kumuondoa mamlakani Rais Ibrahim Boubacar Keïta mwezi Agosti mwaka jana na Rais wa mpito, Bah Ndaw, mwezi Mei mwaka huu, hawatakabiliwa na mashitaka.

Hoja hiyo ilipitishwa kwa wingi wa kura za wabunge katika baraza la taifa la mpito la Mali.

Kanali Goïta amesema kuwa ataheshimu ukomo wa Februali 2022 , tarehe ambayo aliahidi uchaguzi wa serikali ya kiraia utafanyika.

Chanzo: millardayo.com