Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa upinzani waungana na Ruto kuidhinisha mswada wa IEBC

Ngunyi Adai Ruto Na Raila Kuungana Ni Pigo Kwa Mt Kenya Viongozi wa upinzani waungana na Ruto kuidhinisha mswada wa IEBC

Tue, 9 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi wa Azimio Raila Odinga na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka ni miongoni mwa viongozi ambao wameungana na Rais William Ruto akiidhinisha Mswada wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Hafla hiyo ilifanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta (KICC), hatua kutoka kwa idhini za hapo awali ambazo zimefanywa katika Ikulu.

Hatua hii inakuja kufuatia shinikizo la maandamano ya vijana nchini humo wanaojiita Gen - Z ambapo miongoni mwa mambo madai mengine walimtaka Rais Ruto kuharakisha mchakato wa uundwaji wa IEBC kwa mujibu wa katiba.

Mchakato wa uteuzi wa maafisa wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya unatarajiwa kufuatia baada ya ya kuidhishwa kwa sheria ya IEBC.

Mswada huo ni mojawapo ya utekelezaji muhimu ambao ni matokeo ya mazungumzo ya Kamati ya Kitaifa ya Majadiliano.

Pia walikuwepo Naibu Rais Rigathi Gachagua, na Mwanasheria Mkuu Justin Muturi miongoni mwa maafisa wengine wakuu serikalini.

Kutoka kwa Upinzani, kiongozi wa wachache katika Bunge la Kitaifa Opiyo Wandayi, naibu viongozi wa chama cha ODM Hassan Joho na Wycliffe Oparanya pia walihudhuria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live