Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa mapinduzi Gabon wasema Ali Bongo sasa yuko huru

Viongozi Wa Mapinduzi Gabon Wasema Ali Bongo Sasa Yuko Huru Viongozi wa mapinduzi Gabon wasema Ali Bongo sasa yuko huru

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Viongozi wa kijeshi wa Gabon wametangaza kusitisha kifungo cha nyumbani cha Rais Ali Bongo aliyeondolewa madarakani, wakisema kuwa sasa "yuko huru kutembea apendavyo."

Katika taarifa iliyosomwa kwenye TV ya serikali Jumatano jioni, Msemaji wa Jeshi Kanali Ulrich Manfoumbi alisema uamuzi wa kumwachilia Ali Bongo ulitokana na "hali yake ya afya."

"Anaweza, ikiwa anataka, kusafiri nje ya nchi kwa uchunguzi wa matibabu," aliongeza.

Tangu jeshi lilipofanya mapinduzi Agosti 30, lilimweka Rais huyo wa zamani katika kizuizi cha nyumbani, na kutangaza kuwa wanadhibiti nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta.

Uamuzi wa kumwachilia huru unafuatia shinikizo kutoka kwa jumuiya ya kikanda ya Afrika ya Kati ECCAS na majirani wa Gabon, kuheshimu uadilifu wa kimwili wa kiongozi huyo wa nchi aliyeondolewa madarakani.

Mnamo 2018, Ali Bongo alipatwa na kiharusi. Afya yake ilikuwa chanzo cha wasiwasi kwa wengi katika maandalizi ya uchaguzi wa Rais wa 2023.

Chanzo: Bbc