Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa mapinduzi Gabon wamteua Jenerali Nguema kuwa kiongozi mpya

Viongozi Wa Mapinduzi Gabon Wamteua Jenerali Nguema Kuwa Kiongozi Mpya Viongozi wa mapinduzi Gabon wamteua Jenerali Nguema kuwa kiongozi mpya

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: Voa

Maafisa wa jeshi walionyakua mamlaka katika mapinduzi nchini Gabon siku ya Jumatano wamemtaja Jenerali Brice Oligui Nguema kuwa kiongozi wa mpito wa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Jenerali Nguema hapo awali alibebwa kwa ushindi katika mitaa ya mji mkuu Libreville na wanajeshi wake.

Rais aliyeachishwa madaraka, Ali Bongo, ameonekana kwenye video akiwa nyumbani kwake, akitoa wito kwa “marafiki zake duniani kote” “wapige kelele” kwa niaba yake.

Koloni la zamani la Ufaransa ni mojawapo ya wazalishaji wakuu wa mafuta barani Afrika.

Chanzo: Voa