Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa kikatoliki Afrika wapinga agizo la Papa la kubariki wapenzi wa jinsi moja

Viongozi Wa Kikatoliki Afrika Wapinga Agizo La Papa La Kubariki Wapenzi Wa Jinsi Moja Viongozi wa kikatoliki Afrika wapinga agizo la Papa la kubariki wapenzi wa jinsi moja

Fri, 12 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Maaskofu wa Kanisa Katoliki barani Afrika wamepinga tamko la Papa Francis la kuwabariki wapenzi wa jinsi moja wakidai kuwa ni kinyume na mapenzi ya Mungu.

Kongamano la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar(Secam) - Muungano wa Maaskofu wa Kikatoliki kote Afrika - ulisema katika taarifa kwamba hatua ya Vatican kubariki wapenzi wa jinsi moja "haifai".

"Mafundisho ya mara kwa mara ya Kanisa yanaelezea vitendo vya wapenzi wa aina hiyo kuwa 'vya kuchukiza' na kinyume na sheria ya asili.''

Rais wa Secam, Kardinali Fridolin Ambongo, alisema ujumbe huo umeidhinishwa na Papa Francis na wataendelea na ushirika wao na mkuu wa Kanisa Katoliki.

Mwezi uliopita, Papa Francis alitangaza kwamba makasisi wanapaswa kuruhusiwa kuwabariki wapenzi wa jinsi moja.

Hili limezua hisia tofauti kutoka kwa Kanisa Katoliki na jumuiya ya LGBT.

Lakini Vatican ilisema baraka hazipaswi kuwa sehemu ya taratibu za kawaida za Kanisa au zinazohusiana na miungano ya kiraia au harusi.

Iliongeza kuwa msimamo wa kanisi ni kwamba ndoa ni ya kati ya mwanamume na mwanamke.

Kuna nchi 64 ulimwenguni ambazo zinaharamisha mapenzi ya jinsi moja na karibu nusu ya hizi ziko barani Afrika.

Chanzo: Bbc