Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa Umoja wa Afrika walaani hujuma za Israel dhidi ya Gaza

Umoja Wa Afrika Israel.jpeg Viongozi wa Umoja wa Afrika walaani hujuma za Israel dhidi ya Gaza

Sun, 18 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika uliokuwa ukifanyika mjini Addis Ababa Ethiopia, wamelaani vikali kile walichokiita "hujuma ya Israel" katika Ukanda wa Gaza na kutaka kukomeshwa mara moja vita.

Sambamba na kulaani hujuma na uvamizi huo wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza, viongozi walioshiriki mkutano wa Umoja wa Afrika huko Addis Ababa Ethiopia wametoa mwito wa kukomeshwa mara moja jinai za Israel dhidi ya Wapalestina.

Akihutubia katika mkutano huo, Moussa Faki, Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, alilichukulia shambulizi la Israel kuwa ni ukiukaji wa kikatili zaidi wa sheria za kimataifa za kibinadamu na akasema: Tel Aviv inataka kuwaangamiza wakaazi wa Gaza.

Huku akitangaza mshikamano wa nchi za Umoja wa Afrika na watu wa Palestina, Faki alisisitiza: Tunalaani vikali mashambulizi ya utawala wa Israel dhidi ya watu wa Gaza, ambayo hayajawahi kutokea katika historia ya wanadamu.

Moussa Faki, Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika,

Rais Azali Assoumani wa Comoro aliyemaliza muda wake kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) sambamba na kupongeza shauri la mashtaka ya Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) amebainisha: Kwa bahati mbaya, jeshi la utawala wa Israel linafanya jinai na mauaji ya halaiki huko Gaza mbele ya macho yetu.

Azali Assoumani ambaye leo amekabidhi uwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika kwa Rais wa Mauritania ameitaka jamii ya kimataifa kutofumbia macho dhulma, mauaji na ukandamizaji unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live