Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa Seneti walumbana

89878 Seneti+pic Viongozi wa Seneti walumbana

Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Washington. Viongozi wa vyama vya Republican na Democrats katika Bunge la Seneti nchini Marekani wamelumbana kuhusiana na kanuni zitakazofuatwa katika kesi inayomkabili Rais wa nchi hiyo, Donald Trump.

Democrats wanataka hakikisho kwamba mashahidi na baadhi ya nyaraka muhimu zitaruhusiwa ili kuruhusu kile ambacho wanakitaja kuwa kesi ya haki.

Kiongozi wa Democrats, Chuck Schumer amesema ufichuaji wa barua pepe kuhusu msaada wa Ukraine ni kumbusho kuhusu kwa nini uwazi unahitajika.

Lakini hakukosa kukubaliana kuhusu iwapo mashahidi wataruhusiwa kutoa ushahidi wao wakati wa kesi hiyo.

Rais Trump alipigiwa kura ya kutokuwa na imani naye katika Bunge la Wawakilishi wiki iliyopita kwa matumizi mabaya ya madaraka na kulizuia Bunge hilo kufanya kazi yake.

Hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa kwamba hataondolewa madarakani kwa kuwa chama chake cha Republican kina maseneta wengi katika Bunge hilo ambako kesi hiyo itaendeshwa kulingana na Katiba.

Kesi hiyo inatarajiwa kuanza mwezi ujao baada ya likizo kukamilika. Lakini wana Democrats hadi sasa wanakataa kutoa nyaraka za kesi hiyo katika Bunge la seneti.

Wanataka hakikisho kutoka kwa McConnell kwamba mashahidi wao waliowachagua, karibia wanne wakiwa wafanyakazi wa sasa na wa zamani wa Ikulu, wenye ufahamu kuhusu kilichotokea Ukraine, wataruhusiwa kutoa ushahidi.

Hata hivyo, McConnell alisema hawajakataa mashahidi na kwamba atasimamia kesi kama ile iliyomkumba aliyekuwa Rais wa Marekani, Bill Clinton mwaka 1999, ambapo maseneta waliamua ni mashahidi gani watakaoitwa baada ya kufungua mjadala na maswali.

McConell alimshutumu Spika wa Bunge la Uwakilishi, Nancy Pelosi kwa kushikilia nyaraka hizo na kwamba anajaribu kutuelekeza jinsi ya kuendesha kesi hiyo katika Seneti.

Chanzo BBC Swahili

Chanzo: mwananchi.co.tz