Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa ODM Kilifi mbaroni

Hukumu Pc Data Viongozi wa ODM Kilifi mbaroni

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

eshi la Polisi limewakamata viongozi wanne wa ‘Orange Democratic Movement’ (ODM) Kaunti ya Kilifi, mjini Mtwapa, wakiwa katika kujiandaa kuwaongoza waandamanaji na kwamba watu hao wanashikirikiwa katika kituo cha Polisi Kilifi.

Waliokamatwa ni pamoja na Spika wa Bunge la Kilifi, Teddy Mwambire, lakini pia yumo Mbunge wa Kilifi Kusini, Ken Chonga, Msaidizi wa Seneta wa Kilifi, Patrick Chiro, pamoja na Victor Katana, Ofisa katika ofisi ya Mbunge wa Kilifi Kusini.

Kwa mujibu wa mtandao wa Taifa Leo, Seneta wa Kilifi, Stewart Madzayo, amefanikiwa kukwepa mtego huo wa Polisi waliokuwa wakimwandama, kwani lengo la Jeshi hilo ni kujaribu kukabiliana na walio katika mstari wa mbele kuandaa maandamano Kilifi.

Akizungumza na wanahabari katika kituo cha Polisi cha Kilifi, Mbunge Chonga ameeleza kuwa walikuwa wanajiandaa kuwahutubitia wakazi waliojitokeza kushiriki maandamano kabla ya kuanza maandamano yenyewe katika eneo hilo.

“Jana Jumanne tulisema wazi tutaandaa maandamano ya amani na Polisi wametukuta tukiwa tumekusanyika, tayari kuwahutubia waandamanaji. Wao wakashikilia lazima watu watawanyike. Tumejaribu kuwafafanulia ni muhimu tuwahutubie wafuasi wetu wakati Polisi wenyewe wakiwepo, lakini kumbe walipanga njama wawatawanye kisha watukamate sisi viongozi,” amesema Chonga.

Leo Jumatano maandamano yaliyoitishwa na kiongozi wa Azimio La Umoja One Kenya Raila Odinga yameshika kasi katika maeneo mbalimbali nchini.

Mnamo Jumanne muungano wa Azimio ulishikilia kwamba maandamano yatafanyika leo Jumatano, kesho Alhamisi na Ijumaa.

Muungano huo unasema Serikali ya Kenya Kwanza imepandisha gharama ya maisha na kwamba wakenya wengi hawezi kumudu bei za juu za bidhaa za msingi kama unga, mafuta ya kupikia na sukari.

Pia viongozi wa Azimio wanasema kupandishwa na kuongezwa kwa tozo na kodi kunafanya maisha kuwa magumu zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live