Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wajadili hali ya usalama DRC

Fg UfssWQAEAI1T.jpeg Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wajadili hali ya usalama DRC

Tue, 8 Nov 2022 Chanzo: Bbc

Marais wa Burundi, Tanzania, Kenya na Rwanda pamoja na Waziri mkuu wa DRC wamekutana kando na mkutano wa COP 27 Sharm El Sheikh Misri kujadili hali ya usalama mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mazungumzo hayo yaliyoongozwa na Mweneykiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye yanakuja baada ya mazungumzo yake na mpatanishi katika mchakato wa mazungumzo ya amani ya mashariki mwa Congo rais wa zamani wa Kenya uhuru Kenyatta, yaliyofanyika mjini Bujumbura wiki iliyopita.

Haya yanajiri huku hali ya wasi wasi ikiendelea kutokota baina ya DRC na Rwanda huku kila upande ukipande ukimshutumu mwenzake kuwaunga mkono wapinzani wake.

Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo inaishutumu Rwanda kuwaunga mkono waasi wa M23 walioteka hivi karibuni baadhi ya maeneo ya mashariki mwa Congo, huku Rwanda ikiishutumu DRC kwa kuunga mkono kundi la wapiganaji wa- Kinyarwanda wa FDLR wanaoshutumiwa kufanya mashambulio kwenye maeneo yaliyo karibu na mpaka ndani ya Rwanda. Kila upande unakanusha madai hayo.

Jumatatu Rwanda iliishutumu DRC kwa kuingiza ndege yake ya kijeshi Rwanda na kulaani kitendo hicho kamacha uchokozi. DRC ilikiri kuingiza ndege hiyo, lakini ikasema kuwa haikuwa na nia mbaya.

Chanzo: Bbc