Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa Jubilee kujadili kumuunga mkono Raila

A1ed5455c63e48fa Viongozi wa Jubilee kujadili kumuunga mkono Raila

Thu, 14 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wakati uchaguzi mkuu wa 2022 unapokaribia, imekuwa dhahiri kwamba kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga amejitokeza sana katika Mlima Kenya.

Wakazi wa eneo hilo ambao kwa miaka na mikaka wamekuwa wakimwona kama adui yao wa kisiasa kwa siku za hivi karibuni wamkuwa wakiyeyusha mioyo yao na kumkumbatia.

Leo, wajumbe wa jubilee kutoka maeno bunge 12 ya Kiambu walitangaza kumuunga mkono Raila katika azma yake ya kuchukua uongozi baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2022

Wakazi wa eneo hilo ambao kwa miaka na mikaka wamekuwa wakimwona kama adui yao wa kisiasa kwa siku za hivi karibuni wamkuwa wakiyeyusha mioyo yao na kumkumbatia.

Leo, wajumbe wa jubilee kutoka maeno bunge 12 ya Kiambu walitangaza kumuunga mkono Raila katika azma yake ya kuchukua uongozi baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Katika mkutano uliaondaliwa eneo la Jumuia Conference and Country Home, Limuru na gavana wa Kiambu Dkt James Nyoro, wajumbe walijitolea kufanya kampeni za nyumba hadi nyumba kumtafutia kura Raila ambaye walimtaja kama mwenye maendeleo.

Nyoro amezungukwa na sehemu ya MCAs na wenyeviti wa chama cha jubilee kutoka maeneo 12 ikiwa ni pamoja na Ruiru, Juja, Lari, Kiambu Town, Limuru, Kikuyu, Kabete, Kiambaa, Githunguri, Mji wa Thika, Gatundu Kusini na Gatundu Kaskazini.

Katibu Mkuu wa Chama hicho Mary Kirika aliwachambua viongozi ambao alisema wamekuwa wakimdharau Mwenyekiti wa Kitaifa wa chama hicho, Rais Uhuru Kenyatta.

Alisema kuwa Uhuru ni Mfalme wa mkoa wa Mlima Kenya na atabaki kuwa simba wa mkoa huo hata baada ya kustaafu kutoka ulingo wa siasa mwaka ujao.

"Tutafuata mwelekeo ambao Uhuru atatuonyesha. Ingawa hajasema waziwazi, vitendo vyake vinazungumza hata zaidi kuliko maneno," alisema.

Aliongeza kuwa kwa wale wote wanaotembelea mkoa huo kutafuta kura za urais wanapaswa kufanya hivyo na baraka za Uhuru.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke